Insha ya asiyesikia la mkuu huvunjika guu

Jamii ya kiafrika, hasa waswahili, imejaa hazina kubw ya metha zinazobeba mafunzo muhimu kwa vizazi. Mojawapo ya methali hizo ni “Asiyesikia la mkuu huvunjika guu”. Mehali hii inatufundisha kuwa mtu asiyesikiliza ushauri ya wazee au watu wenye uzoefu zaidi, hungia katika matatizo makubwa ambayo angeweza kuyaepuka. Insha hii itachambua maana ya methali hii, itatoa mfano wa adithi unaodhihirisha ukweli wake, na hatimaye itatoa mafunzo tunayopaswa kuyazingatia.

Methali hii ina maana ya ndani. Kimaana halisi, mtu anayekataa kusikiliza maonyo ya wazee a u wakbwa wanaomtahadharisha kuhusu hatari fulani, mwisho wake anaweza kupata madhara ya kimwili, kama kuvunjika guu. Hata hivyo, maana ya ndani ya methali hii ni kubwa zaidi: inatufundisha kuwa ushauri na maonyo ya watu wazima, vingozi, au wenye uzoefu, hutokana na hekima na maarifa waliyoyapata kwa muda mrefu. Kukataa kuyasikiliza ni sawa na kujiandalia mateso au majuto ya baadaye.

Hadithi inayodhirisha Methali

Hapo zamani za kale, katika kijiji kimoja, aliishi kijana mmoja aliyeitwa juma.Juma alikuwa kijana mwenye nguvu na kipaji, lakini alikuwa na tabia ya kutosikiliza ushauri wa wazazi na wazee wa kijiji chake.

siku moja, wazee wa kijiji walimwonya juma asiende kuvua samakia ziwa fulani wakati wa msimu wa mvua, kwani maji huwa na mkondo mkali na hatari ya kuzama huwa kubwa. Walimweleza kuwa wavuvi wengi waliokuwa wamakaidi onyo hilo hapo awalu walipata madhara makubwa

Juma hakuwasikiliza. Aliwaona wzee kama watu wa kizamani wasioelewa mambo ya sasa. Siku moja, alipanda mtumbwi wake peke yake na kuelekea kilindini bila kumjulisha mtu. Ghafla bin vuu, dhoruba kali ilitokea na mkondo wa maji ukamsukuma mtumbwi wake dhidi ya mawe makubwa. Mtumbwi ulipinduna na juma akaanguka majini, akiumia guu lake vibaya alipogongana na jiwe.

Wavuvi wenzake waliomsikia akipiga kelele walimwokoa na kumfikisha hospitalini. Baada ya wiki kadhaa za matibabu, jum alijifunza somo kubwa nmaishani mwake: Ushauri wa azee haupaswi kupuuzwa.

Mafunzo Tunayopata

Hadithi ya juma inatuonyesha wazi kuwa ushauri wa wazee, vingozi, na watu wenye uzoef unatokana na uchunguzi na uzoefu wa muda mrefu. Kukaidi ushauri huo bila sababu za msingi kunaweza kutuletea madhara amabayo tungeweza kuyaepuka kwa urahisi. Ni vyema kila mmoja wetu, hasa vijana, tujifunze kusikiliza na kuzingatia maoni ya wale wanaotujali na kutuonya kwa nia njema.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top